I received this poem in Swahili and I would like to share it as it reflects on Ramadan. I wish everyone a Ramadhan Makbul.
YA RABBI UTUNUSURU
Ninaanza kwa salamu, Baraka nizifaidi
Nashika yangu kalamu,Kusema imenibidi
Enyi ndugu isilamu, Umati wa Muhamadi
Ya Rabbi utunusuru, Pepo tusijeikosa
Mikono naifungua, Na kwa moyo mkunjufu
Mgeni ameshatua, Mwezi mwema mtukufu
Naupokea kwa dua, Na furaha sufu sufu
Ya Rabbi utunusuru, Pepo tusijeikosa
Mwaka huu mtihani, Si rahisi ni mgumu
Kuifunga Ramadhani,Mchana kutwa saumu
Kwa kweli sio utani,Yapaswa kujilazimu
Ya Rabbi utunusuru, Pepo tusijeikosa
Daku msilisahau, Mkatafuna vitende
Ugali au pilau, Msipokula ni mbinde
Mujipige angalau,Saumu isiwashinde
Ya Rabbi utunusuru, Pepo tusijeikosa
Mchana jua ni kali, Lazima kuvumilia
Magharibi nayo mbali,Adhana kusubiria
Ukahisi huna hali, Na ari kukuishia
Ya Rabbi utunusuru, Pepo tusijeikosa
Sio matumbo pekee, Nafsi pia fungani
Macho msikodolee, Maovu kuyatamani
Ubora ni mtembee, Mkitazama angani
Ya Rabbi utunusuru, Pepo tusijeikosa
Tena nchi za ulaya, Mazingira ni hatari
Watu wamekosa haya, Kwa kupenda ufahari
Tabia zao ni mbaya, Kwao kufunga hiari
Ya Rabbi utunusuru, Pepo tusijeikosa
Hiyo miji ya likizo, Msimu wa kiangazi
Ndio kuna matatizo, Wanawake wote wazi
Kuvaa sio kigezo, Vimini ndio mavazi
Ya Rabbi utunusuru, Pepo tusijeikosa
Tumuombe Maulana, Ya Allah ya Karimu
Tusijeipata lana, Kwa mambo yaso muhimu
Tutendeni ya maana, Isitupate hukumu
Ya Rabbi utunusuru, Pepo tusijeikosa
Tamati nimefikia, Imepita alasiri
Magharibi meingia, Namalizia shairi
Wenzangu nawakimbia,Nenda tafuta futari
Ya Rabbi utunusuru, Pepo tusijeikosa
by Hamza A. Mohammed
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
2 comments:
Wow sis long time no see. Ramadhan Kareem tena Mungu akubarikie mengi.
Salaam dear,
it's nice to see you too. Nipo bwana siku hizi zaidi kwenye blog ya mahanjumati...good eatings namiss chakula cha home.
Post a Comment